[.:ENGLISH:.|.:ITALIAN:.|.:FRENCH:.|.:SWAHILLI:.|.:HINDI:.    
 
 


 

News letter subscription
   
Name
Email
 

 

 

 

 

 

 

 

 

NI WAJINGA TU HUFA

Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu….Mimi nimesema, ndinyi miungu, na wana wa Aliye juu, nyote pia. Lakini mtakufa kama wanadamu, mtaanguka kama mmoja wa wakuu.

PDF

Ni wajinga tu hufa; hili lawezakuwa ni jambo nzito kidogo kwa wengi kwa sababu, la kwanza, linawezasikika kama kiburi na majivuno mwanadamu anaposikia likisemwa lile, ambaye, pamoja na ulimwengu aliomo yeye mwanadamu, unatukuza sana kifo na hata ule ulimwengu hufanya maagano na kifo. Ndio, kwa njia moja au nyingine, wanadamu wamekitukuza kifo, kukiinamia, na hata bila kujua wakasema, “ewe kifo, nani kama wewe!”

Kabla yako kukasirika na kunipuuzilia mbali, utazame ule mstari tena; “Ni wajinga tu hufa” na kile Yesu alisema alipowaambia wayahudi wa kale, “walio wafu na wazike wafu wao”. Hili lilikuwa ni jibu lake kwa mtu ambaye kwa unyonge na upole alimwomba akaweze kumzika babake, halafu aje amfuate Yesu.

Kama wayaelewa waliyoyafanya wayahudi walipokuwa wanawazika wafu wao, pamoja na sheria zilizoambatana na hayo za urithi, utaelewa ni kwa nini huyo kijana mdogo alikwazika. Inamaanisha kuwa wao, na vizazi vilivyokuwa mbele yao, Musa akiwemo, walikuwa ni wapumbavu, wasiokuwa na maarifa, ambao walifungwa na tamaduni za kuwazika waliokufa. Huyu kijana myahudi ambaye kwa muda aliuona mwanga wa Nuru yake Yesu, na akatafuta kuyaambatonisha maisha yake na hiyo Nuru, kwa ghafula anashtuliwa na usemi wake Yesu, na anarudi kwenye kiza na asihesabiwe kati ya wafuasi waliomfuata Yesu, na basi kuipoteza nafasi yake kwenye Mkono wa Kuume wa Utukufu.

Yesu, kama mwingine yeyote aujuae Ukweli na kutembea kwenye kwenye Nuru hatakuwa na lolote liambatanalo na ulimwengu uegemeao kifo na kuzimu.

Yesu hangekubali kuambatanishwa na hekaya na hadithi za kuomboleza zitokazo kenye mavumbi ya makaburi, ila Yeye angeimba pamoja na mbele ya ndugu zake katika nchi ya walio hai, wakiunena Upendo wa Baba Yake aliyembariki na Baraka zote rohoni na akampa vitu vyote kwa furaha yake. Alifunuliwa ili akafichue vilivyofichika katika hali za kishetani na akavimalize kupitiamoto wa miguu Yake iletayo Injili, kuwafungua ndugu zake kutoka kwa nira ili kuingia kwa uhuru mkuu wa (M)wana wa Mungu.

Kwa ajili hii sauti kuu itokayo mbinguni, ikiambatana na ngurumo na radi kwa walio kwenye nchi yasema, "Agano letu na kifo litavunjwa na makubaliano yako na kifo hayatasimama tena". Ni sauti hiyo hiyo ingurumayoiliyonena kupitia Yesu katika siku zake za mwili na inayoongea wakati na majira haya kupitia malaika (mitume) wake Mungu ambao wameambatana na kweli.

Kwa kweli, kubarikiwa ni wale ambao hawatakwazwa na Nuru hata inapozima na kudunisha tamaduni na taratibu za mababu zilizokwezwa na mipangilio ya wanadamu wa ulimwengu huu wa nje tuishio kati mwake; nah ii Nuru yafanya vile kwa kumfunua Yeye Yule, Pweke Aliyekatikati ya mambo yote.

Heri mtu Yule ambaye hana mashaka nami - Luka 7:23

Kumbuka kuwa, kumjua Huyu Ambaye Yohana amwashiria anaposema ‘lazima akwezwe name nidunishwe’, ni lazima nishushwe mimi mwenyewe katika utu wangu, na jumla ya imani zilizoko ndani ya utu ule ziwe bure. Dunia lazima ijae na maarifa Yake Huyu kama vile maji huijaza bahari, kwa sababu kando Yake hapana mwingine; hii ndio Siku ya Yeye Aliye, wakati ambao kila vuli litatoweka na kutokomea na Yeye Aliye kudhihirika. Tunaposimama kwenye Nuru, inadhihirika kwamba mambo yote yaliyo nje yake ile Nuru ni vivuli tu na mafumbo. Ukiliona, kuligusa, kuliita, kulionja, ujue kwamba hilo ni vuli na ni fumbo na linamwashiria Yule Aliye sirini. Mwanadamu awezakuwa mjinga, abebaye mizigo isiyostahili, mchovu na mwenye uchungu kwa njia zote zile anapovikimbiza vivuli kila siku ya maisha yake. Katika Nuru, kila kitu ambacho wanadamu hukishikilia kama cha dhamana katika ulimwengu huu tuliomo, kwa ghafula hufanyika vinyago vichukizavyo na sanamu, kwa sababu havijakitwa katika kweli.

…kwa maana kile kinachoonekana kuwa kitukufu mbele ya watu, Mungu anakiona kuwa takataka - Luka 16:15.

Na kama tujuavyo, mara kwa mara, Yesu alikumbwa na pingamizi kutokana na watawala na wafalme wa ulimwengu huu ambao hawangestahimili mafunzo na mafundisho yake yaliyofunza kuwa kuna Mungu tu, na Yeye Yesu ni mmoja na Mungu. Kwa nini hili liwakwaze watu? Hili fundisho takasika linalomfunua Mungu kama yote ndani ya yote ni kama Jiwe litupwalo, lililokatwa kutoka Milele ila sio kwa mkono wa mwanadamu, na kuharibu na kutawanya uvumbini kila msingi wa imani za wanadamu walizojikweza kwazo.

Katikati ya mojawapo wa nyakati zile za kupingwa kwake, Yesu, kwa upole aliwakumbusha watesi wake kwamba yale maandiko waliyoyashikilia kama jiwe-msingi na kina cha imani yao, yakiri peupe kuwa wao wenyewe ni miungu, na wana wake Mungu Aliye Juu zaidi. Yesu alikuwa akisema kwa udhahiri kuwa, "Ndugu zangu, mmesahau kuwa sisi ni hali moja, Baba Mmoja, Uhai Mmoja, Utukufu Mmoja; mmesahau kuwa pale mwanzo tulishangilia kwa furaha pamoja katikati ya wana wake Mungu, na vile tuliimba kwa sauti zenye utamu kati ya nyota za asubuhi".

Badala ya kuwatuliza, kuwakomboa na kuwaponya, hiyo miale ya Nuru ya ufunuo halisi itiririkayo kutoka kwenye vilindi vyake Baba ilipepeta miale ya moto wa kuwauguza na hasira hata walipotafuta kumsulubu Kristo. Lile neno lililokuwa kama umande kwa mche mchanga, lilikuwa liwaletee ukumbusho na kuwainua hadi hatima ya utukufu wao, lakini kwa ghafula likawa kikwazo kwao, na uvundo mkuu wa kifo ukafanyika. Wakawacha rehema iliyokuwa iwaletee wokovu, na kwa kufanya lile, wakamsulubu Yesu Aliyekuwa Uhai Wao, kwao. Hawangewezaelewa na kuikumbatia ile Nuru inayong’aa kwenye lile shimo lililo kenye fahamu zao zenye kutiwa kiza, na kufuatia lile, wakafa kwa sababu ya kutoamini kwao kama wanadamu tu wa kawaida. Hiyo Nuru ilikuwa iwakomboe kutokana na nira ya kifo na iwape nguvu tena na zaidi kuwa wana. 

Ana mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda…Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu. - Yohana 1:12.

Mwanadamu awezaje kwa ujinga na upofu kuukataa wokovu mkuu namna hii unaotangazwa leo kwa kila kiumbe kilichoko chini ya mbingu. Mtu awezawanyoshea kidole cha lawama waliohifadhi torati ya Musa na imani ya Kihebrania nyakati za Yesu ilhali wao washindwa kutafakari kwa undani. Hii ni nia ya waandishi wa torati na mafarisayo inayodhihirisha fikra za mwanadamu zilizokita mizizi na kufunganishwa na mambo makuu ya kishetani, na ambayo hayawezikuzielewa siri za Uzao Wake Mungu, ambazo zimefichika chini ya vuli za mifano tofauti ya wanadamu na miigo ionekanayo na isiyoonekana. Ndio nia ile ile iliyonyonge na isahauyo, inayoelekea kwa ubatilifu wa mambo ya kijinsia ambayo hata Yesu mwenyewe alipigana nayo aliposimama katika pengo na kuifunua ile siri ya Uungu wetu.  Ndio nia ile ile inayojidhihirisha kama shetani, itafutayo kumvutia na kumjaribu Mwana kupitia utukufu wa ulimwengu upitao umfanyao yeye kuiacha hali yake ya kwanza, na kuukimbilia utukufu wa ulimwengu Alipofunga. Baadaye, Yesu alisema, "…kwa maana roho i radhi lakini mwili ni dhaifu", kwa maneno mengine, ni nyonge na dhaifu kusikia na kuelewa mambo makuu ya Mungu.

Akiandika kupitia kuongozwa na Roho, mwandishi wa Zaburi 82 azungumzia kuhusu siri kuu, KUSANYIKO LA MWENYE NGUVU – MUNGU MWENYE NGUVU. Mwandishi wa Zaburi hii fupi alifunguliwa macho kuona kitu ambacho yeye mwenyewe hakukielewa; alikuwa akiliangalia Kusanyiko – Kanisa – Kusanyiko kutoka Dunia yote – Kusenyiko la Miungu katika Jina la Baba. Haijanakiliwa kuwa Kusanyiko litakuwa kwake Bwana; ni hivyo kwa sababu hilo Kusanyiko lilitokana na, na Chanzo Chake ni Yeye Bwana. Hawa ndio haswa walio Mungu…Mwili wake Mungu; wanao ukamilifu wa hali yao umefichika ndani Mwake Mungu, maana kuwa wao waishi kwa niaba ya, na kupitia Yeye. Hawa ndio wale Kusanyiko linalojitokeza kama Wingu juu ya maji likikiri, “na kuwe…”, “natu…” Ndilo Kusanyiko la Mungu anayejitokeza tena kama Mtu wa Kibingu asemaye, "Mimi Ndiye Mwenye Mamlaka yote, niishiye milele, na pweke aliye nazo fungua za kuzimu na za kifo”. Kuhusu huu umati wa wana wa Mungu yesu asema, kifo hakina nguvu; kwa maneno mengine, hawawezi kufa.

Yesu atukumbusha tena kuwa tulikuwa katika hilo kusanyiko la Mwenya Nguvu na Milki Yote anaposema, "Ulikuwa Nami tangu mwanzo" (Yohana 15:27). Kama hili laashiria chanzo cha kila mwanadamu, basi kwa nini mwanadamu afa?  Kwa nini waonekana kama wamepungukiwa na hatima ya kilele cha Mungu? Zaburi 82 inatupa jawabu lililo rahisi: "Hawajui, wala hawatafahamu; watembea katika kiza: pale “…misingi yote ya nchi imetikisika". Twawezahatimisha haya kwa misemo mitatu, ‘bila maarifa’, ‘bila kuelewa’, ‘upofu rohoni’. Yadhihirisha upumbavu wa kiroho uliowakamata wanadamu walio kwenye ulimwengu huu ambao wanaipoteza milki yao ya kiungu. Katika kutoelewa kwao na kutiwa kiza, wamefanyika tu watu wanaokufa na kwa hivyo wao wafa kama wanadamu. Nalafu baada ya pale yasikika sauti ya mzika wafu ikisema, “nyinyi ni mavumbi…..”

Watu wangu huangamia kwa kukosa maarifa: kwa sababu mmeyakataa maarifa (Hosea 4:6)

Twaweza sasa kuelewa ya kuwa (m)wana wa Mungu Aliye Juu ni wa ile hali isiyoharibika nay a milele kama Babaye wa Mbinguni, na kupitia lile, kifo hakiwezimshikilia. Baba wa Nuru yote asema, “ndani mwangu sina kifo, kwa hiyo siwezikitoa nisocho nacho, mbali mimi hukifufua kilichokufa na kukisafirisha hadi Uzimani. Katika Ufalme wangu uharibifu haujawahisikika; hakuna kidanganyacho katika Ufalme wangu.” Kinachozaliwa na Mbegu isiyoharibifu pia ni kisichoharibika na cha umilele na huzaa matunda yaambatanayo na ule Uzima kulingana na mfano wake.

Mjinga ni nani, isipokuwa yeye aiachaye hali yake ya kwanza kwa kutoyahifadhi maarifa ya Bwana wa uhai wake. Akikiri kuwa yeye ni mwenye hekima katika njia za kilimwengu, yeye basi huiondokea kweli na maarifa ya Hali yake halisi, Bwana asiyeonekana na asiye na uharibifu, na kuibadili kwa kile kinachoharibika. Ni hali ile ile katika habari ya wana wa Mungu nyakati zake Nuhu waliodanganywa na ubatili wa mali (ambao ni ukawaida), wakaiacha hali yao ya utukufu na kushuka ili kuungamanika na walio na mwili, na baadaye wakafutiliwa kuingia vilindini vya njia za mauti. Wakijidhania kuwa wenye hekima, wakafanyika ukamilifu wa ujinga wakijiharibu wenyewe kwa kuuwacha utukufu wa maarifa ya Mungu Muumba wao na kujiambatanisha na kilichoumbwa, na ndicho chanzo cha kufa kifo cha wanaadamu. Yasikie maneno yake Roho: "itamfaidi nini mwanadamu akijitwalia taifa na utukufu wa ulimwengu huu tu na kuipoteza nafsi yake kwa nguvu za kaburi?"

Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo. Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. - Zaburi 14:1-2.

Yatafakari haya, hakuna hata mwanadamu mmoja chini ya mbingu anawezajisitiri kutokana na ubatili huu wa kuyakataa maarifa Yake Mungu. Kama wangeyahifadhi haya maarifa Yake Mungu hawangekuwa watu wafungwao duniani. Badala yake wangekuwa wana wake Mungu walio na kweli ya uzima wao ndani Yake katika mbingu. Makaazi yetu halisi ni ni Ndani Yake, katika mbingu, ambazo ni Ufalme wake Mungu. Tunapojua haya, kama Yesu tunawezasema bila tone lolote la shaka kuwa sisi si wa ulimwengu huu tulio: Hata ingawa kwa muda tunawezapatikana ndani yake, sisi sio wa ulimwengu huu. Kwa ajili ya hili pekee, mtumishi wake Mungu anatangaza Habari Njema na ya Milele ya Upatanisho kwa waishio ulimwenguni ambao wamepotoka na kuiondokea hali yao ya mwanzo ndani Yake Mungu, akisema, “tubuni na mkamrejelee Bwana wa Uzima wenu; mkapatanishwe Naye ili muokolewe”.

Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye injili ya milele, awahubiri wao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji. - Ufunuo 14:6-7.

Tambua kwamba hii injili njema imeelekezwa kwa wale wanaoishi ulimwenguni wala sio kwao wanaoishi katika mbingu ambamo linapatikana Kanisa. Kupatikana, au kuishi ulimwenguni kwa hakika yamaanisha kuwa wa kilimwengu, kijinsia na kuwa na nia batilifu ya kiwanadamu, ambayo ndio maana yake kifo. Habari Njema ni kwamba imeundwa kiasi kwamba inaleta uvuvio, nuru na upatanisho, ili wana wake Mungu wakawezejitambua tena katika uridhi wao katika kusanyiko la kibingu lake Mungu.

Wana wake Mungu, amkeni toka wafu na mkaamini tena katika lile Jina Moja; kwa imani mkabatizike katika hio utambulisho huo wa Bwana wa Utukufu. Mkaipokee Habari Njema ya Neema inayofunua huu ushirika uliofichika ndani Mwake Mungu, ambao hata wewe ni mshirika. Usikie ujumbe wake mtumishi na uishi.

Akinena kwa Jina la Baba, Yesu aliendelea kukiri, "awaye yeyote asiyeamini kwamba Mimi Ndiye, atafa katika dhambi zake". Linganisha maneno haya yake Yesu na hili: "mshahara wa dhambi ni mauti". Kupitia yote haya, tunapata kuona kuwa Yesu anatupa maana mpya ya dhambi, inayofutilia mbali kile ambacho wanadamu waliita dhambi. Na ndicho hiki; Dhambi ni kukosa kwake yeyote kujitambua katika ukweli na utambulisho wake halisi kama mwanaye Mungu ambaye ndiye mmoja naye Baba. Ni kama kujiambatanisha na hali nyingine ambayo ni ubinafsi wa kimwili. Kutoamini pekee ni dhambi, na ndio maana anasema, “Amini na uokolewe”. Uamini nini? Uamini kuwa Yeye Aliye, Ndiye Yuko ndani yako na Yeye Ndiye ayaaye sayari yote. Ukawezaamini hili, unaweza basi kuingia katika Upumzisho Wake kama vile Mungu Mwenyewe alivyopumzika, kwa sababu jangwa la uharibifu, ambalo lalinganishwa nakutoamini labadilishwa kuwa Shamba liotao mema – Edeni. Mtoe adanganyaye, asemaye uongo na uamini tena.

Kutoamini huleta kifo, hali iendeleayo na kumwangusha asimamaye kutoka kwa Chanzo chake, "BWANA MUNGU WAKO"; ni mwanguko usiokoma unaoelekeza kwenye shimo la utupu ambamo kujua kilichochema na kirembo, na chenye utukufu wa Uzima wa Mungu hupotea. Mwanadamu asipojitambua kuwa mwana mpendwa wake Mungu, ampendezaye na asiyehukumika mbele Zake, yeye ataadhirika na kuugua katika mateso yaongezekayo ya mauti na kifo. Kushindwa kuyasikia maagizo na maelekezo yanayosaidia kumtafuta Mtakatifu Aliye Ndani, ambaye chanze Chake ni Umilele, humfanya huyu mwana kufa kama mwanadamu. Akizidi kuishi katika ubatili huu wa kutokumbuka mahali pake katika zile nyota za sayari zizungukazo, ataishi kutangatanga katika kiza kisichoisha, mbali na mahali pake pafaapo katika vilele vitakatifu Vyake Mungu, mahali pa nguvu zote.

Yatafakari haya, "…kwa sababu ya upendo usiopimika Wake Mungu kwa ulimwengu, Amemtoa Mwanawe Pekee ili ulimwengu ule usiangamie”. Ulimwengu ni ule ulioondokea ukweli wa ushirika wa umoja wake Baba na Mwana na kwa hilo kufanyika kipofu kwa ile kweli kuwa “MIMI NDIYE”; hii ndio maana ya kifo. Mwanadamu awezajepindua au kuigeuza hii hali? Ni rahisi, kuipokea karama yake Mungu bure, ambayo sio lingine ila kukubali kuwa yeye ni Mwana. Na kwa utiifu kuifuata Sauti ya Yule Upako na kuzifungua ile mihuri iliyoifunga fahamu yako; mkubalishe aliye Ndani ainuke na atokeze. Usimwache adanganyaye adanganye tena, mfurushe autawalaye ulimwengu huu apingaye kurejea kwako kwa mahali pako pafaapo katikati mwa Edeni.

Ukawe na furaha kila wakati kwa sababu Baba wa Nuru yote ametupa nuru, itufanyayo wenye hekima machoni pake. Cha kustaajabisha ni kuwa hiyo hiyo hekima tunayoipokea kutoka juu kila wakati itasikika ni kama ujinga kwa walio nje kwa sababu imefichika kutoka kwao. Walio na hekima machoni pa Mungu, hata ingawa wao huonekana wakiwa wajinga na wapumbavu kwao walio nje, wao huivumbua njia ya utakatifu kuurejelea Uzima, mahali ambapo kifo hakipo tena. Wao husimama milele kwenye patakatifu wakiwa wajitambua tena katika Bwana. Ndani Yake hamna kifo tena, wala tunda lake ambalo ni huzuni, uchungu na kuomboleza; nao huu ndio Uzima wa Milele. Inuka na ufufuke kutoka kwa wafu na ukatawale katika Uzima; furahia haya!

Ana hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hoa; wasifirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. Hapo hawatakuwa na samba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. Na hao waliokombolewa na bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.- Isaya 35:8-10

 

Wenu,

Trevor Eghagha, wa Huduma ya Sunray.

www.sunrayministry.org